Loading...
 

Maamuzi na Kupata Alama za Mdahalo

 

Matokeo ya mdahalo wa Agora sio "Kushinda" au "Kufeli", lakini kupewa tuzo ya maalum ya idadi za pointi kulingana na jinsi timu yako ilivyokuwa na ushawishi.

Mfumo wa alama utatakiwa kuundwa pale sheria zote zitakapokuwa tayari, lakini miongozo hii ya msingi itatumika: 

  • Kukubali POA na Kuunganisha Timu kunatakiwa kuhimizwa sana (na kwahiyo alama kupewa kwa timu zote) ili kuipa uzito mwingi kujenga makubaliano na kutafuta madaraja kuliko uadui.
  • Kutambua uwongo kwenye hoja za timu nyingine kunatakiwa kupewa alama.
  • Kusoma dondoo mara kwa sana kunatakiwa kuadhibiwa, haswa kama mwanachama wa timu anasoma kutoka kwenye hotuba iliyoandikwa kabla.
  • Kutowasilisha ushahidi, au kutoa ushahidi ambao haupo kunatakiwa kuadhibiwa vikali, na kutambua hiko kunatakiwa kupewa tuzo kubwa.
  • Tabia zisizokubalika zinatakiwa kuadhibiwa vikali.

Inapendekezwa pia kuwa kila mwanachama wa Agora ana alama yake binafsi ya mdahalo ambayo inahimiza ushiriki. Mfumo huu, hata hivyo, hautakiwi kuwa wa kuongezeka tu ili kutoweka kizuizi kwa wanachama wapya.

 

 


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Tuesday August 17, 2021 20:28:11 CEST by zahra.ak.